Ukumbi  Wa Mashirikiano Duniani – Nairobi

 

Kwa Jina La Mungu

 

Kuwakumbuka walioadhiriwa na siasa kali za Kidini

 

Tahadhari! Msalaba Utavumbuliwa!

 

+            Msalaba huu unapinga ugandamizaji dhidi ya utumiaji wa vibonge vya kuzuhia uzazi na elimu ya uzalishaji.

 

+            Msalaba huu haubagui dhidi ya utuoji mamba au sayansi ya utafiti wa uzazi bila ngonobali unaotetea haki za wanawake wote duniani

 

+      Msalaba huu umeundwa na Msanii Jens Galschiot kutoka Denmark.

 

Twahijitaji wasaidizi na watu ambao tuweza kufanya nao duniani, wasililiana kwa njia ya barua pepe – aidoh@aidoh.dk ama anagalia www.aidoh.dk/InTheNameOfGod

 

Sanamu Hii ya Msalaba

Huu msalaba unatokana na sanaa ya uchongaji na ni sanamu tu. Sanamu hii imechongwa kwa kutumia nishani ya shaba nyekundu na imebandikwa jina ‘In the Name of God” (“Kwa Jina La Mungu”). Huu msalaba ni chombo kinachowakilisha haki za kutumia vibonge vya kupanga uzazi na kutokuwa na ubaguzi dhidi ya elimu ya uzazi.

 

Historia

Tangu jadi, msalaba kama sanamu umetumiwa vibaya na wanaoipinga bibilia kwa kusema kuwa bibilia inakubali ngono bila ukingaji. Katika hii sanaa, sanamu hii inaonyesha kijana wa makamo ambaye si mweupe au mweusi na ambaye ni mjamzito. Kijana huyu ametundikwa msalabani akisulubiwa. Hadhma yake kuu ni kuchangia katika mjadala kuhusu vidonge vya kuzuhia uzazi (contraceptives) au uabaguzi dhidi ya elimu ya kizazi iliyochangiwa na sayansi (stem cell research) na si siasa kali za kidini (religious fundamentalism).

 

Kwa mara ya kwanza sanamu hii ilionyeshwa katika Kanisa Kuu lililoko katika mjii mkuu wa Denmark, Copenhagen mnamo tarehe 01.12.2006. Mkuu wa kanisa hilo Bw. Anders Gadegaard alinukuliwa akisema:

 

“Tunaungana na wasanii walioichonga sanamu hii hili kuthibitisha kuwa sisi hatuungani kamwe na wanaokataa bibilia kuchangia katika mjadala wa utumiaji wa vibonge vya uzazi katika mjadala wa upangaji uzazi na elimu ya uzalishaji”

                        (Tafsiri)

 

Msalaba huu utavumbuliwa sehemu mbali mbali hapa Nairobi wakati wa mkutano wa kimataifa wa kushirikiana (World Social Forum). Baadaye utafumbuliwa huko Vatican, Marekani na nchi zingine ulimwenguni.

 

Huu ni msalaba unaotetea haki za kutumia vibonge vya kupanga uzazi.

 

Rais wa Marekani Bw. George w. Bush na wakuu wa Kanisa la Kikatoliki wameungana kusurutisha ulimwengu mzima kuaamini kuwa kinga ya pekee dhidi ya uneeezaji wa maradhi ya ukimwi na mimba ovyo ni kutoshiriki katika ngono. Tayari, msimamo huu wao usio na msingi wa kisayansi umechangia kubuniwa sera mbaya barani Afrika, Asia na Marekani ya Kati ambako mamilioni ya watu wameadhiriwa na ukimwi, maradhi ya zinaa na utoaji wa mamba. Maoni zaidi kutoka Vatican yanaweza kupatikana katika mtandao www.vatican.va .

 

Msanii Jens Galschiot

Jens Galsciot alizaliwa 1994 huko Odense Denmark. Anajulikana sana kutokan na kazi zake za kipekee zinazoegemea tofauti za kiuchumi kote ulimwenguni. Kazi zake  za sanaa zimewahikuonyeshwa katika bara la ulaya (European Cities ’93), Hong Kong, Mexico na Brazil.

 

Miradi yake inafadhiliwa mauzo ya sanaa yake na michango kutoka kwa wafadhili wa kibanfsi, mashirika yasiyo ya serikali na vyama vya wafanyi kazi.

 

Bw. Galschiot amenukuliwa akisema:

 

“Sanamu hii haipingani na dini ya kikristo ulimwenguni. Nakubiliana na wote wanoyachukua maadili meme ya bibilia. Hata hivyo, sanamu hii kamwe haikubaliani na wanoegemea siasa au tafsiri kali ya bibilia ambayo ndio imeendelea kuchangaia masaibu mengi dhidi ya watu wengi duniani.

 

Pia sanamu hii haisemi utuoaji wa mamba uhalalishwe. Inatetea haki zinazoambatana elimu bora ya uzazi” (Tafsiri)

 

 

Mkutano (World Social Forum)

Kutakuweko na sanamu mbili katika mkutano wa Nairobi unaoanza tarehe 20.01.2007. Pamoja na wasanii kutoka Kenya Uganda, kutakuwa na asana ya uigizaji na mijadala kuhusu swala hili.

 

Mchango na Ushirikiano

Mradi huu unahitaji msaada na/au mchango wa wafadhili, washirika na wasanii kote ulimwenguni. Msaada huu utawezesha msalaba huu kuzulu nchi zingine ulimwenguni hili kuboresha mjadala wenyewe.

 

Tunatarajia kuwa mashirika ya wanawake, vijana, sanaa, au yale yanayohusika na sera ya upanganji uzazi, uteteaji wa haki za kibinadamu, vyama vya kisiasa na watu binafsi watependezwa, kuuchangia na kuusaidia mradi huu.

 

Mradi huu umebuniwa na wasanii wanaojitegemea na ambao hawana mlengo wowote wa kisiasa au kidini. Kazi yetu inahitaji wahisani, washiriki na wasanii kamaa wewe.

 

Unaweza kuufuatilia mjadala wa sanamu hii kwa kuuangalia mtandaowetu ambao ni www.aidoh.dk/InTheNameOfGod au www.aidoh.dk/GlobalGag kwa habari zaidi za kimataifa. Ama, jiunge nao kwa kutaandikia barua pepe katika aidoh@aidoh.dk

 

www.aidoh.dk/wsf2007 Wakati wa mkutano wa Nairobi Msanii Jens Galschiot anaweza kupigiwa simu katika nambari 0728 947 393 au 0728 947 390 au kwa barua pepe aidoh@aidoh.dk

 

 

Jens Galschiot – sculpteur, Banevaenget 22 – DK-5270 Odense N – Danemark

Tél.+45 6618 4058 – Fax +45 6618 4158

Email: aidoh@aidoh.dk – Internet: www.aidoh.dk